Namwachia Lyrics
[Verse]
Yangu furaha, Imegeuka majuto
Kicheko kimegeuka kilio
Ila ninaamini wema hauozi umenipa mazito, me naumia hey
Nilijua utanifuta machozi umenipa majonzi, me nalia
[Pre-Chorus]
Zangu hisia nilishindwa kuficha
Wazi wazi ukatambua
Na Ndonga ukanpasua
Wangu rafiki, Wote ulowajua
Na Nguo ukawavua, Pasipo me kujua
Wacha nikae pembeni
[Chorus]
(Namwachia Mungu tu)
Labda kuna mahali nilikosea
(Namwachia Mungu tu)
Kesi yako kwake nakushtakia
(Namwachia Mungu tu)
Maana umezidi kunionea
(Namwachia Mungu tu aaaahh)
[Verse]
Nilikupa Muda na vyote vilivyo vyangu
Ila malipo ya yote kunitukanisha na ndugu zangu
Kweli mzoea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi
Nimelijua sawa
Moyo wangu umeuchakaza
Umehondomola mpaka gunzi
Wema umenilipa ubaya
Sitoshindwa hata tukionana
Kuachana sio uhasama
Sintothubutu kuzozana nimekunawa
Nakuombea kheri salama
Umpate yule mtakae wezana
Kumbuka kugunga zipu bwana msije kwazana
[Pre-Chorus]
Zangu hisia nilishindwa kuficha
Wazi wazi ukatambua
Na Ndonga ukanpasua
Wangu rafiki, Wote ulowajua
Na Nguo ukawavua, Pasipo me kujua
Wacha nikae pembeni
[Chorus]
(Namwachia Mungu tu)
Labda kuna mahali nilikosea
(Namwachia Mungu tu)
Kesi yako kwake nakushtakia
(Namwachia Mungu tu)
Maana umezidi kunionea
(Namwachia Mungu tu aaaahh)
Song Tags
Comments (0)
📌 By commenting, you agree to follow these rules. Let’s keep PearlTunes, Africa a safe and vibrant place for music lovers!